HABARI NZURI YA MTANDAO WA KUCHANGIANA FEDHA KWA HIARI DUNIANI KOTE.

VITA, UJAMBAZI NA UGAIDI MWISHO WAKE UMEFIKA!

Kila kilicho na mwanzo hakikosi kuwa na mwisho. Yale mataifa yanayopigana vita sasa, yaache vita hivyo mara moja. Na kuanza kuelewana kwa kuanzisha urafiki mzuri wa kufanyiana biashara za kiserikali za nchi hizo zinazopigana vita. Na biashara hizo zitaleta uchumi wa maendeleo ya hali ya juu zaidi kwa pande zote husika. Pia na watu wa nchi hizo nao wataanzisha biashara zao za kununuliana na kuuziana bidhaa ana kwa ana. Pia na kwa biashara za mawasiliano ya mitandao ya simu za mkononi. Maana vita hivyo wanavyopigana sasa, vimepitwa na wakati sana, kulingana na elimu ya sayansi ilivyo na mavumbuzi yake ya teknolojia iliyo na maajabu makubwa, ya habari nzuri mno za hadithi zilizobuniwa kwa mafundisho ya ufundi wa kumaliza vita, ujambazi, ugaidi na umasikini kwa muda wa mwaka mmoja duniani kote.

Maana dunia kwa sasa ni kijiji kimoja, au nyumba moja kwa mawasiliano ya simu za mkononi. Kwa hali hiyo kama jambo fulani likitolewa kupitia kwa vyombo vya habari, na kwa mitandao ya kijamii, litajulikana kwa siku moja au siku mbili, duniani kote. Yatupasa tukumbuke sasa kuwa; nchi ya Ujerumani zilikuwa nchi mbili tofauti, lakini zilipoungana kuwa nchi moja. Kwa sasa ni nchi moja wapo iliyo na uchumi mzuri sana wa kimaendeleo katika eneo la Ulaya.

Kulingana na hali hiyo, leo chanzo kikuu cha umaskini duniani ni mawazo mabaya yanayotokana zaidi sana kwa pande zote husika, maskini na matajiri. Dunia leo ina watu matajiri wengi mno wa hali ya juu zaidi, na wa hali ya kati, ambao matajiri hao wakiamua kwa muda wa mwaka mmoja ulimwenguni kote, wanaufutilia mbali kabisa umaskini ili usionekane usoni pa dunia hii, kwa kila mtu mwenye akili timamu ya kufanya kazi, kama vile kilimo, na ufugaji wa mifugo, au ufundi, na biashara mbalimbali n.k. njia rahisi ya kumaliza haraka zaidi umaskini. Vita, ujambazi na ugaidi duniani kote. Kuna njia moja maalumu ambayo inaelezwa ndani ya kitabu cha Biblia pekee. Nayo ni kusaidiana kwa hali na mali kwa kila mmoja. Mafungu ya Biblia yanayosema watu wasaidiane na kuchangiana fedha ni haya yafuatayo:-

Waefeso 4:28. Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji. Matendo 2:45. Waliuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja.

Luka 6:38. Wapeni watu vitu nanyi mtapewa kipimo cha kujaa na kushindiliwa! Mathayo 6:33. Utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. Kitabu cha Biblia kimejaa habari za utajiri mtupu wa Mungu, na uzima wa milele. Utajiri huo wa Mungu ni wakupindukia mipaka ya utajiri duniani. Achana na ule utajiri wakujulikana kwa kijiji kimoja, au mtaa mmoja, Utajiri wa Mungu ni wa kujulikana kiwilaya, au kimkoa, ama kitaifa, na kimataifa! Soma wewe mwenyewe. Kumbukumbu 28:12-13. Malaki 3:10. Waefeso 3:8-9. Njia ya kuupata utajiri huo wa kupindukia mipaka ya utajiri. Kama ilivyoelezwa hapo mwanzo wa habari hii kuwa, tuwe na Mungu kwanza, tumwamini Yesu na kabatizwa kama Yesu alivyobatizwa katika mto wa Yordani. Marko 1:9-11 pili kuanza kumwomba Mungu mara kwa mara bila kuchoka, huku tukimtolea shukrani za kila wakati, kwa kadri anavyotulinda, na pia azidi kuendelea kutulinda, ili na haja zetu tulizonazo zijulikane kwa Mungu. Wafilipi 4:6-7. Yafaa kwa siku kupiga magoti mbele za Mungu kumuomba Bwana tuwe ndani ya nyumba, mara 4. Au mara sita. Usiku wa manane, asubuhi, mchana na jioni. Wakati mwingine tuwe na maombi ya siri ya rohoni bila kufahamu watu wengine kuwa unaomba Mungu Mathayo 6:5-6, Waefeso 6:17-18.

Roho ya shetani muda wote huwa inakuja kumjaribu mtu hata kama amelala usingisi usiku, au mchana. Ama hata awe kwa watu wengi, au kanisani, au anasafiri kwa bus, ama kwa gari, au ndani ya ndege. Mawazo mabaya huwa yanakuja tu ya kila namna. Mtu anapoingiliwa na mawazo mabaya wakati huo huo amwombe Mungu ayaondoe mawazo mabaya ya kila namna. Kama mawazo hayo yatakuwa yakiendelea ndani ya roho ya akili ya mtu. Naye aendelee tu kuomba kimoyoni kuwa: Bwana naomba uniondolee mawazo mabaya haya kwa jina la Yesu, mpaka pale tu yatakapoisha.

Biblia inasema ombeni bila kukoma. 1 wathesolonike 5:7. Jambo la kuomba, hata kama mtu awe kwenye kazi yoyote aendelee kuomba Mungu kimoyoni. Neno la Mungu lasema; Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo mithali 4:23. Chanzo cha matendo mabaya ni mawazo mabaya. Wakristo wengi waliomwamini Yesu imekuwa ni vigumu sana kupata mibaraka mikubwa ya kutoboa kupata utajiri mkubwa, kwasababu bado mawazo mabaya wanayaruhusu yakae ndani ya roho zao kwa muda mrefu, wakiwaza mawazo mabaya kila wakati bila kuyazuia kwa neno la Mungu. Kwa kuomba mfululizo kimoyoni ili wasifahamu watu wengine kuwa unaomba Mungu. Ikiwa kama mtu yuko kwa watu wengi. Zaburi 66:18-19. Mithali 6:16-19. Upande mwingine mawazo mabaya yanazuia sana kujibiwa maombi kutoka kwa Mungu, pia mawazo mabaya ni chanzo kikuu cha mikosi mikubwa sana duniani. Tena watu wengi zaidi huwa hawajuwi kuwa mikosi mingi huwa inatokana na nini? Lakini kadri mtu anavyowaza mawazo mabaya ndivyo na mikosi itakavyokuwa ikimfuata popote pale. Maana wengine huwa na mawazo mabaya ya kutamani wanawake na wanawake kutamani wanaume, wakati wanawake na wanaume hao sio wake wao au waume wao rasmi mithali 6:20-29. Au Mithali 6:32. Mathayo 5:28 watu wengine uingiliwa hasira kali ya mawazo mabaya ya kutaka kupiga watu, au kutukana watu, pamoja na mawazo ya uchoyo na kiburi cha dharau. Watu wengine huwa wakiwaombea watu wenzao wapatwe na mabaya. Mathayo 5:44-45.

Wapo watu duniani watakaojaa mawazo mabaya sana ya kishetani asiye na huruma. Wataupinga utaratibu huu mzuri unaoelezwa ndani ya kitabu cha Biblia wakuchangiana fedha kila aliye na shida ya fedha. Mathayo 15:19. Mfano; kwa ajili ya kuanzisha mradi wa kilimo cha umwagiliaji wa maji kwa mashamba, na upandaji wa miti mingi ili kutunza mazingira na uoto wa asili ili uendelee kuwepo pamoja na ufugaji wa mifugo. Pia na kuchangiwa ili kupata fedha kwa ajili ya elimu ili kuendelea kusoma zaidi kwa wale wanaohitaji elimu n.k.

Yapo mafungu mengi ya Biblia yanayosema wakristo wazidi kusaidiana kwa hali na mali kwa upendo wa Mungu. Maana Mungu ni upendo. Soma 1 Yohana 4:8. Tena 1 Yohana 4:20. Pia 1 Yohana 3:15. Kwa hali hiyo. Watu wakipendana vizuri watachangiana fedha kupitia simu za mkononi, au Bank kwa kila anayeomba kupitia kwa vyombo vya habari, kama vile radio, TV, magazeti au kwa mitandao ya kijamii ya facebook, whats App, Instagram, Tiktok, au kanisani, ama kwa kikundi cha watu wengi watakaoelewana kuchangiana kila mmoja, au sehemu ya kijijini, au kwa mtaa Fulani n.k

Kama mtu Fulani atatumiwa fedha na watu milioni 3 kupitia kwa simu yake. Tufanye mfano huo, kila mmoja achangie fedha 500. Ukifanya mahesabu ya watu hao milioni 3. Zitakuwa ni fedha nyingi mno za mabilioni! Naye aliyechangiwa atachangia watu wengi zaidi. Kama itakuwa Hivyo tunachosubiri nini sasa watu kuanza kuchangiana fedha kila mmoja kuanzia sasa. Au bado Yule shetani asiye na huruma anatukalia kimawazo ili tusielewe njia iliyo rahisi, na ya haraka zaidi. Na pia ni nzuri na salama. Na ya thamani kubwa kama jiwe la dhahabu lililo na uzito wa kilo elfu 50.

Maana utaratibu wote huo wakuchangiana fedha unataka kila mtu awe na kazi maalumu iliyo nzuri ya kumpatia kipato cha fedha kama vile kilimo, ufugaji wa mifugo, au biashara na ufundi n.k. ndipo mtu apate fedha ya kumchangia mtu mwenzake. Soma Waefaso 4:28. Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele. Bali afuataye mambo ya upuuzi atapata umaskini wa kumtosha. Mithali 28:19. Tena mithali 10:4 linganisha na 2 wathesalonike 3:10.

Yatupasa tuelewe kuwa fedha na dhahabu ni mali ya Mungu, pia nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana. Dunia na wote wakaao ndani yake. Zaburi 24:1. Kama fedha na dhahabu ni mali ya Mungu kwa nini baadhi ya watu huwa wanakataa kuwachangia watu wenzao, kana kwamba fedha hiyo walio nayo watakaa nayo milele na milele bila kufa. Uchoyo ni kitu hatari sana. Ndiyo maana vita haviishi duniani. Uchoyo wa namna hiyo unahitaji huruma za Mungu zipatikane kwao. Kitabu cha Biblia kina habari nzuri sana zinazoelezea ukweli unaotakiwa ufanywe na watu wote wanaoisoma Biblia, na kuielewa vizuri. Lengo lake kuu ambalo tunatakiwa tuwe na maombi mengi ya kila wakati. Hiyo ndio kazi ya kwanza tuliyopewa na Mungu ya kuomba mara kwa mara kwa Mungu bila kuchoka soma Luka 18:1-8.

Yesu alikuwa akiomba mara kwa mara. Luka 5:16. Tena Luka 6:12. Yesu alikesha usiku kucha akimwomba Mungu. Pia soma Luka 22:44. Pili yafaa tuwe wasomaji wa Biblia vizuri. Tatu tuwe wahubiri wa injili ya Neno la Mungu. Na njia za kuhubiri Neno la Mungu zipo za aina nyingi, kwanza; kazi tunazofanya kila siku, kama vile kilimo, biashara na ufundi n.k. kilimo tukilima kwa mafanikio makubwa yakupata mazao mengi zaidi. Hapo itaonyesha kuwa sisi tuko pamoja na Mungu. Kazi hiyo ya kilimo na biashara mbalimbali zilizo nzuri, pia na ufundi itakuwa moja wapo ya kuhubiri injili ya Yesu.

Njia nyingine ya kuhubiri, tuwe na tabia nzuri za kusaidia watu wenye shida mbalimbali kama vile wagonjwa, wenye njaa, na walio na hali ya umasikini. Pia na kusaidiana sisi kwa sisi kwa kuchangiana fedha kila anayehitaji fedha ya kuanzisha mradi wa jambo lolote lililo zuri kama vile kujenga nyumba, kilimo, biashara n.k. kwa hali hiyo itakuwa ni vizuri, Warumi 15:26. Kwa upande wa utoaji wa zaka na sadaka, kama watu wengi watalielewa vizuri somo hili la kuchangiana fedha kwa kila mmoja, watu wengi wa mamilioni na mabilioni watatuma fedha nyingi sana za zaka na sadaka kwenye makao makuu ya makanisa yao. Zaka na sadaka hizo zitajaa na kufurika kama mto wa maji unavyotiririka maji mengi, baada ya mvua kubwa kunyesha. Na mahesabu ya namba za zaka na sadaka hizo; wakati mwingine zitakuwa hazina namba za mahesabu ya binadamu duniani. Maana zitakuwa ni nyingi mno zisizopimika kimahesabu. Hii ndio italeta Baraka kubwa kwa wakristo wote duniani!

Kuhusu habari za Biblia ni nzuri, pia neno lake ni tamu kuliko asali Zaburi 19:10. Tuache kuzipinga habari za Biblia kwa mawazo mabaya ya uchoyo na kiburi cha dharau. Soma Yakobo 2:15. Ikiwa ndugu mwanamme au mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki, na mtu wa kwenu akawaambia endeni zenu kwa amani mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwili yafaa nini? linganisha I Yohana 3:17. Mtu akiwa na riziki ya dunia hii. Kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake. Je, upendo wa Mungu wakaaje kwa mtu huyo?

Leo hii kwa dunia ya sasa, kama mtu Fulani tajiri akijitokeza aanze kuwahamasisha watu waanze kuchangiana fedha. Kwa kila anayehitaji fedha kupitia kwa vyombo vya habari, na kwa mitandao ya kijamii, huku pia akiwaasaidia wenye shida mbalimbali, kama vile wagonjwa, wenye njaa. Na walio na hali ya umasikini kwa kuwapa mitaji ya fedha ili wakaanzishe miradi mbalimbali kama vile ya kilimo, biashara, au ufugaji wa mifugo. Mtu huyo kama ataendelea kufanya Hivyo. Mashirika makubwa duniani ya kimataifa yatampatia zawadi ya nobel ya mabilioni ya dola, kama vile Mama Teleza wa India alivyopatiwa zawadi ya nobel, kwasababu alikuwa akisaidia sana watu waliokuwa na hali ya umaskini. Kulingana na habari hii iko wazi kwa kila mtu atakayejitoa kusaidia watu kwa hali na mali, awe mtu mmoja, au wengi. Ama kikundi cha watu, au serikali yoyote. Ama Rais wa nchi yoyote ile, akisaidia watu walio na hali ya umaskini na kuwa matajiri wakubwa, na nchi yake inakuwa ya amani na usalama zaidi na kuanza kuwahamasisha watu kuchangiana fedha kwa hiari na upendo, kama wanavyofanya kampeni za uchaguzi wa viongozi. Naye Rais huyo upo uwezekano mkubwa wakupewa zawadi ya nobel kwa haraka bila kuchelewa. Kulingana na habari hii ni nzuri tujihusishe watu wote kuchangiana fedha kila anayehitaji fedha za kuanzisha miradi ya maendeleo ya kuleta utajiri kwake, na kwa watu wengine, ili tuweze kuvimaliza vita vyote vinavyopiganwa duniani kote, pamoja na ujambazi, wizi, na ugaidi wa kimataifa. Leo watu wengi wanaangamia kwa sababu ya kukosa maarifa ya upendano wakusaidiana kwa hali na mali. Hosea 4:6. Kama watu wanaangamia kwa sababu ya fedha dawa yake ni fedha, na neno la Mungu. Ikiwa watu wengi watalielewa vizuri somo hili la kuchangiana fedha kwa kila mmoja kupitia simu za mkononi, tutakuwa matajiri wote, watu wenye akili timamu.

Na tutatembea katika miji mikuu na midogo bila wasiwasi wowote ule, na mali zetu zote, iwe mchana, au usiku ulimwenguni kote! Leo duniani tuko watu wengi mno wasiopungua bilioni 6. Lengo lake kuu Mungu aliwaumba watu wawe wengi namna hiyo ili wawe wakisaidiana kwa hali na mali, sio kwa kupigana vita, na kuchukiana. Mwanzo 9:1-2. Kama watu ndio tuko wengi namna hiyo. Kwa watu bilioni moja, au zaidi ya bilioni 2, waamue kumchangia mtu mmoja au zaidi ya watu wengi. Nikiwa na maana ya kwamba; kwa kila saa watu milioni 2 wawe wamechangiwa na watu walio zaidi ya bilioni 2 kupitia simu za mkononi kwa kiasi cha fedha ndogo ndogo tu isiyoleta hasara kwa mchangiaji. Je, hali ya umasikini itakuwa bado inaendelea duniani? Jibu rahisi unalo wewe mwenyewe. Mungu atubariki tuwe na ufahamu wa kuelewa somo la habari hii. Mtu mmoja mwenye hekima na busara anaweza kuuliza swali la kuwa kama watu wote duniani tutakuwa matajiri wote. Ni nani sasa atakayefanya kazi za shambani, au viwandani na kwa maofisi ya serikali, na hospitalini au ufundi wa kujenga nyumba, na ufundi wa umeme, na magari, au ndege, meli na tren, na ufundi wa kompyuta na simu, pia na TV. Na udreva wa magari ya aina yote. Pamoja na kuchunga ngombe n.k.

Jibu ni kwamba; shughuli zote hizo zinazofanywa na binadamu duniani kote. Akili ya AI, ambayo watu wengine wanaiita, akili mnemba, au akili ya kubuni. AI artificial interlligance itafanya kazi zote za aina yoyote ile zinazofanywa na binadamu sasa, hata ziwe za ualimu, pia na kuandika kwa kompyuta za aina zote hata ziwe za simu n.k. pia akili hii ya AI Mungu akipenda hivi karibuni nayo sio ajabu inaweza kuanza kuongoza biashara ya masoko ya hisa ya kimataifa ya ubadilishaji wa fedha (Forex) akili ya AI inaweza kuimarisha biashara hiyo ya forex inakuwa ya kuleta faida siku zote, kwa wawekezaji, wa aina yote ile. Hata wawe wamewekeza fedha ndogo au nyingi wote watakuwa wakipata faida kubwa zaidi kila dakika, kila saa kila siku, kila wiki, kila mwezi.

Itakuwa hakuna kupata hasara hata kidogo, maana biashara hiyo itakuwa ikiongozwa na akili ya AI. Lakini hata Hivyo, kama itatokea hasara kwa bahati mbaya. Kwa kuwa akili ya AI itakuwa kwenye shughuli zote za uchumi duniani kote kama vile kwa makampuni makubwa mbalimbali, na kwa mabenki ya bima ya biashara ya Forex yaliyo na AI yatalipa hasara hiyo itakayotokea kwa bahati mbaya, endapo hao watakaolipwa hasara itakayotokea, wawe mitaji yao inapitia kwenye mabenk ya Bima ya forex yatakayoanzishwa yakiwa na akili ya AI.

Kuhusu habari hii ya masoko ya kifedha ya kimataifa yaani ya ubadilishanaji wa fedha (Forex) na hisa. Kadri habari hii itakavyokuwa inajulikana ulimwenguni kote, kupitia kwa vyombo vya habari na kwa mitandao ya kijamii, kuanzia sasa, biashara hiyo ya forex na hisa itaanza kuleta faida kubwa kila siku bila hasara, maana wataalamu wa shughuli hiyo, Mungu wa huruma nyingi wanaweza wakaweka maroboti yaliyo na akili ya AI, yatakayoiongoza biashara hiyo ili isitokee hasara kwa wawekezaji wa mitaji ya fedha kupitia kwa mabenki ya bima ya forex, yatakayoanzishwa duniani. Maana akili ya AI ipo kuanzia sasa.

Kama Mungu akipenda matajiri wa shughuli ya Forex waanzishe bank za bima za forex, zikiwa pamoja na akili ya AI. Ili kuongoza utaratibu wote wa kupata faida kubwa zaidi ya mtaji wa fedha utakaowekwa na muwekezaji. Mfano mtu awekeze dola 200, kwa uongozi wa akili ya AI, kwa siku moja itakuwa ikipatikana faida ya dola 5000 au dola 10000, kwa sababu masoko ya hisa ya kununua na kuuza yako mengi duniani kupitia kwa mabenk ya ubadilishanaji wa fedha kama vile dola, ural, au pound n.k masoko hayo ya hisa ya forex yako New york, na Washigton Marekani, Tokyo Japan, Paris Ufaransa, London Uingereza, ujerumani na uholansi na kwingineko duniani kote.

Kulingana na biashara hiyo, wale watakao jiunga na biashara hiyo ya forex kupitia simu zao za mkononi zile kubwa watapata faida kubwa zaidi kwa muda wa miezi mitatu, au sita wanakuwa na mamilioni ya fedha za dola au ural na pound, ambapo wengine watakuwa wameanza na dola 500 au 200. Kama biashara hiyo itakuwa ya kuleta faida kubwa namna hiyo kwa muda mfupi Hivyo ya nini kwa sasa watu wanasumbuka na kuendelea kupigana vita duniani na kufanya ujambazi wa kupora fedha za watu mbalimbali. Baadhi ya watu wengine uamua kufanya mapinduzi ya nchi Fulani. Au kuanzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe. Na unapoangalia vita Hivyo vinavyoanzishwa ni vya maslahi ya kutaka kupata fedha na uchumi wake kwa njia ya vita.

Kulingana na mawazo mazuri ya Mungu waache vita Hivyo mara moja. Badala yake walio na uwezo wa kifedha waanzishe utaratibu wa kuwahamasisha watu waanze kuchangiana fedha kwa kila mtu, au kujiunga na biashara ya Forex ya kimataifa itakayokuwa na akili ya AI. Kulingana na makampuni, na Mabank yatakavyo imarisha biashara ya forex. Akili hii ya AI itakuwa kwenye maroboti ya aina mbalimbali duniani kote, kuambatana na kila kazi inayotakiwa kufanywa kwa hali hiyo watu wote ulimwenguni hawatakuwa na kazi ngumu yoyote, isipokuwa wao watakuwa na shughuli ya kuongoza maroboti ya AI kupitia kwa kompyuta za simu za mkononi n.k ili kutimiza unabii wa Danieli unaosema kuwa siku za mwisho watu wataenda mbio huko na huko na maarifa yataongezeka Danieli 12:4.

Ikiwa unabii huu umeanza kutimia sasa kama alivyoonyeshwa Danieli ni nani kwa sasa anayepinga neno la Mungu na kulikataa, akisema ni la uongo wa kubuni na kutunga habari za uongo. Yeye ndiye muongo mukubwa sana, anastahili apelekwe kwenye anga ya juu ya mwezi akiwa ndani ya Rocket aina ya Apollo22 inayokimbia zaidi ya sauti mara elfu elfu. Akifika huko kwenye anga ya mwezi na kushuka hapo, huku akiwa na ile hewa ya hapa duniani. Atajifunza na kuelewa kuwa, kumbe duniani yupo Mungu wa uzima wa milele. Na pia atakaporudi duniani atautangazia ulimwengu wote kuwa yale maajabu ya Mungu aliyoyafanya kwenye anga ya mwezi yapo mengi! Maana hapo kwenye anga ya mwezi hakuna hewa ya kutembea, au kupumua mpaka uwe na hewa ya hapa duniani! Ndiyo maana ile habari ya kwanza ya hadithi itwayo kwa jina: la

MAAJABU MAKUBWA YATATOKEA DUNIANI! Inasema hivi, hali ya hewa ya anga ya mwezi na hali ya hewa ya hapa duniani, pia na hali ya hewa ya sayari zingine, ikichanganywa kwa elimu ya ufundi wa kisayansi zaidi, inaweza ikatokea hali ya hewa ya muujiza wa kikemia utakaoambatana na nguvu ya miale ya jua itakayokuwa na uwezo wa kuzuia hatari za silaha za aina yoyote ile, ili binadamu asijeruiwe au kuwawa kwa silaha za aina yoyote ile!

Habari hii ya maajabu makubwa yatokea duniani ipo kwa link ya Blog. Ukiandika kwa mtandao wa google hivi, ukubwawamaajabu.blogspot.com kisha unasearch ndipo utaona maandishi ya herufi kubwa yanasomeka THE GREAT WONDERS AI. Yabonyeze maandishi hayo mara moja, au mara tatu au zaidi. Au lile neno kama litatokea lililo na neno sign in, pia nalo libonyeze. Hapo utaona kichwa cha habari kilicho na maandishi, THE GREAT WONDERS HAVE HAPPEN IN THE WORLD!

Yakitokea maandishi ya herufi kubwa za namna hiyo bonyeza maandishi hayo, ndipo itafunguka habari yote ya kingereza na Kiswahili, baadaye utaona neno linalosomeka; Read more nalolibonyeze kisha utaona kichwa cha habari kinachosema; MAANA YA MAKOMANDO WA WILI WASIO NA MIPAKA DUNIANI! Nacho kichwa cha habari hicho kibonyeze, ndipo utakapoona habari yote imefunguka ya maana ya makomando wawili wasio na mipaka duniani!

Je, ndugu msomaji wa habari hii upo hapo, au nimekuacha kwenye mawazo ya ajabu ya dunia hii, nakuomba kwa heshima na tahadhima, jiongeze ili ulielewe soma hili vizuri. Maana umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. Mungu yupo tutashinda matatizo yote ya vita, ujambazi, ugaidi na umasikini kwa jina la Yesu Amina soma Yohana 17:22.


Joseph K. Isamla

Joseph.isamla@yahoo.com

Muleba, Kagera Tanzania

Simu: +255783 486 931


Comments

Popular posts from this blog

WAMTUKANA MUNGU KAMA MTANI WAO!

GREAT WONDERS ARE HAPPENING IN THE WORLD AI! THEY WILL INSULT GOD AS THEIR JOKER.