MAANA YA MAKOMANDO WAWILI WASIO NA MIPAKA DUNIANI.

           

         Ni mfano wa malaika wawili wasio na mipaka ulimwenguni, Yesu alitoa mifano mingi ukisoma kitabu cha Mathayo 13:1-54, kuhusu mfano wa Mabenki ya dunia hii kuwa na fedha nyingi zaidi za kuwakopesha watu wengi kila mmoja za mamilioni ya dola, kupitia simu za mkononi au akaunti benki bila dhamana ya kitu chochote, au watu wakumdhamini mtu, pia na watu wasishike fedha mkononi kama vile noti au sarafu:-

              

          Maana yake ni wale watu watakaomwamini Yesu na kubatizwa na kushika amri kumi za Mungu, huku wakimwomba Mungu mara kwa mara ili Mungu awape mawazo mazuri ya kila wakati na kutenda matendo mazuri, na pia kuwa watoaji wa zaka na Sadaka kikamilifu. Ili zaka na Sadaka hizo zisikae mikononi mwa watu, kama watakuwa na mawazo mazuri kila wakati. Mungu atakuwa tayari kuwafadhiri na kuwakopesha mabilioni ya fedha nyingi mno za dola, au ural n.k maana Mungu anasema; yeye mchana kutwa hufadhiri na kukopesha, soma Zaburi 37:26. Baadaye fedha za Mungu hizo zinaweza kurudi kwa Mungu kama zitatumiwa kwa njia isiyo nzuri, ila kama mtu ataziomba kwa, imani nzuri na kufanya kazi nzuri kama vile kilimo n.k Mungu yuko tayari kumpa utajiri wa fedha nyingi Zaidi! Yale masoko ya hisa ya kimataifa ya ubadilshanaji wa fedha. Forex ni mfano wa makanisa yalioko kwenye Miji Mikuu ya nchi mbalimbali duniani, ambao washiriki wa makanisa hao watakaosoma habari fupi ya hadithi hii na kufuata maelezo yake vizuri. Mungu atazidisha utajiri wao mara elfu elfu. Kama utajiri ukiongezeka Zaidi, washiriki wengine wataanzisha utaratibu wa kutuma fedha zao nyingi za zaka na Sadaka hadi makao makuu ya Makanisa yao kupitia simu za mkononi au akaunti benki n.k.

          

          Na ule mfano wa nyumba 2 za ghorofa 250 kwenda juu zikiwa zimejengwa kwenye mlima wa Kilimanjaro ulioko Tanzania. kuanzia kileleni mwa mlima Kilimanjaro, huku zikilindwa na makomando wawili wa kimataifa wasio na mipaka duniani. Maana yake ni mfano wa watu wawili mme na mke, kama watakuwa waaminifu wazuri kwa Mungu. Bwana Mungu atawabarikia mibaraka mikubwa sana ya utajiri, wanakuwa na maendeleo ya utajiri wa hali ya juu Zaidi kama wamejenga nyumba 2 zao za ghorofa 250 kila mmoja kwenye mlima kilimanjaro.

         Na walinzi hao wawili wa kimataifa wa kikomando wasio na mipaka. Ni malaika wawili wasio na mipaka duniani watakaokuwa wakiwalinda hao mme na mke, watakaokuwa waaminifu kwa neno la Mungu la uzima wa milele. kwa kutoa zaka na Sadaka kikamilifu. Fungua mtandao wa google uandike hivi:ukubwawamaajabu. blogspot.com ukimaliza kuandika hivyo, una search, kisha utaona maandishi yanayosomeka kuwa: GREAT WONDERS AI. yabonyeze maandishi hayo, ndipo itafunguka habari yote tunayo izungumzia kwa mifano mbalimbli. Ikiwa pia ina habari ya wale watakaomtukana Mungu kama mtani wao !

        Biblia inasema itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana Mungu wako kwa bidii kutunza kuyafanya magizo yake yote nikuagizayo leo. Ndipo Bwana atakufunulia hazina yake nzuri, nayo ni mbingu kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake; na kukubarikia kazi yote ya mkono wako. Nawe utakopesha mataifa mengi wala hutakopa wewe. Kumbukumbu 28:8-13. Malaki 3:10. Kuhusu chuo kikuu kitakachokuwa kwenye nyumba mbili zitakazo kuwa juu ya mlima wa Kilimanjaro, ambacho chuo hicho kitakuwa na sehemu ya mafundisho ya kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi, ni mfano mzuri wa chuo kikuu cha Biblia, ambacho chuo cha Biblia kuna masomo mazuri, na mafundisho yanayohusu kufahamu kuwa mungu ana uwezo kwa watu wake watakaomtegemea kwa kumuomba mara kwa mara. 

           Asilimia 100 atawalinda na mabadiliko ya tabia ya nchi, pia atawalinda na aina yote ya hatari kama vile vimbunga, radi za mvua, vita vinavyoanzishwa au ajali, matetemeko ya ardhi, na mafuriko, au sumu ya nyoka n.k Isaya 43:2, Marko 16:17, Mathayo 17:20-21, Zaburi 46: 2-3, tena Zaburi 91:5-8, Danieli 3:19-28. Tena atawalinda na ugaidi, na ujambazi .

           Uwanja wa ndege wa kimataifa utakaokuwa juu ya nyumba hizo, ni malaika watakaofanya kituo cha kushuka na kuruka kwa hao waaminifu wa neno la Mungu zaburi 34:7. Ule uwanja wa kisasa wa kuchezea mpira kidunia: maana yake, niwale wakristo watakao kuwa na neno la Mungu kikamilifu, kwa wale wasio na neno la Mungu,watawaona wakristo wako vizuri kitabia. Na kimawazo, na maendeleo yao yatakuwa yako vizuri, pia na sura zao zitakuwa zinafanana na sura ya Yesu   

            Yale mashirika ya habari ya CNN, na BBC na SKY NEWS, na mengine mengi ni wale washiriki wa Makanisa watakavyoipokea habari fupi hii ya hadithi iliyo na mifano mbalimbali ya neno la Mungu, ambayo kwa uongozi wa Mungu imeandikwa kwa mavumbuzi ya habari za kisayansi na ufundi wake wa neno la Mungu Mathayo 13:52. Yesu akawaambia kwa sababu hiyo kila mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba atoae katika hazina yake vitu vipya na vya kale. kwa hali hiyo kadri wakristo watakavyokuwa wakiieneza habari hii duniani kupitia mitandao yote ya kijamii, au kwa vyombo vya habari. Ndipo utajiri mkubwa wa neno la Mungu utakavyoongezeka Zaidi na Zaidi kwa washiriki wa Kanisa, soma Waefeso 3:8, Wafilipi 4:19. 

              Mibaraka mikubwa kutoka kwa Mungu itapatikana kama mvua ya masika ya Roho mtakatifu kushuka kwa kila atakayekuwa akimuomba mungu kila wakati kimoyoni n.k 1 Wathesalonike 5:17. Wafilipi 4:6-7. Linganisha Waefeso 6:11-18. Isaya 2:4. Habakuki 2:14 na Yoeli 2:23.

               Yesu anasema habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote ; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja Mathayo 24:14.

          

                                             JOSEPH K. ISAMLA

                                             Email : joseph.isamla@yahoo.com

                                                         Simu: +255 783 486 931

Muleba-Kagera-Tanzania

Comments

Popular posts from this blog

GREAT WONDERS ARE HAPPENING IN THE WORLD AI! THEY WILL INSULT GOD AS THEIR JOKER.

WAMTUKANA MUNGU KAMA MTANI WAO!